News

Prof. Mohamed Yakub Janabi Aiwakilisha Tanzania Katika Kinyang’anyiro cha Uongozi WHO Kanda ya Afrika

Prof. Mohamed Yakub Janabi Aiwakilisha Tanzania Katika Kinyang’anyiro cha Uongozi WHO Kanda ya Afrika

Mshauri wa Rais wa Tanzania katika masuala ya afya na tiba ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Mohamed Yakub Janabi, ametangazwa rasmi kuwa mgombea wa nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika. Uteuzi wake unafuatia kifo cha Dkt. Faustine Ndugulile  ambaye alikuwa Mkurugenzi Mteule wa nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyochapishwa kwenye tovuti ya WHO, Prof. Janabi ni mmoja wa wagombea watano wanaowania nafasi hiyo katika uchaguzi ambao utafanyika tarehe 18 Mei 2025 huko Geneva, Uswisi.

Mgombea Pekee Kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara

Katika kinyanganyiro hiki, Prof. Janabi amejitokeza kama mgombea pekee kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara huku wagombea wengine wanne wakitokea Afrika Magharibi. Washindani wake katika uchaguzi huu ni:

  • Dkt. Nda Konan Michel Yao (Ivory Coast)
  • Dkt. Drame Mohammed Lamine (Guinea)
  • Dkt. Boureima Hama Sambo (Niger)
  • Prof. Mijiyawa Moustafa (Togo)

Mchakato wa Uchaguzi na Uamuzi wa Kamati ya Kanda

Mkurugenzi mpya wa Kanda atachaguliwa kupitia kura za wajumbe wa Kamati ya Kanda ya WHO kwa Afrika. Kamati hiyo ilikutana tarehe 14 Januari 2025 ambapo iliamua kutumia utaratibu wa dharura ili kupata kiongozi mpya kwa haraka badala ya kufuata mchakato wa kawaida ambao kwa kawaida huchukua muda mrefu.

Huu ni wakati muhimu kwa Tanzania ambapo iwapo Prof. Janabi atashinda uchaguzi huu basi ataweka historia kwa kuwa Mtanzania atakayeshikilia nafasi ya juu ndani ya WHO Kanda ya Afrika akiongoza juhudi za kiafya barani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top